UTUMISHI CALL FOR INTERVIEW AT MNH, SUA,TPRI,TCAA,SIDO,TALIRI, MDAs & LGAs 12-02-2021

 


JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA
OFISI YA RAIS SEKRETARIETI YA AJIRA KATIKA UTUMISHI WA UMMA.

Kumb.Na.EA.7/96/01/L/36 12 Februari, 2021

TANGAZO LA KUITWA KWENYE USAILI


Katibu wa Sekretarieti ya Ajira katika Utumishi wa Umma kwa niaba ya Hospitali ya
Taifa Muhimbili (MNH), Chuo Kikuu cha Kilimo Sokoine (SUA), Taasisi ya Utafiti wa
Viatilifu na Visumbufu katika Ukanda wa kitropiki (TPRI), Mamlaka ya usafiri wa Anga
Tanzania (TCAA), Shirika la kuhudumia Viwanda Vidogo Tanzania (SIDO), Taasisi ya
Utafiti wa Mifugo Tanzania (TALIRI) na Wizara, Idara Zinazojitegemea, Wakala wa
Serikali na Mamlaka za Serikali za Mitaa anapenda kuwataarifu waombaji kazi
waliotuma maombi ya kujaza nafasi wazi za Taasisi hizo, kuwa usaili unatarajiwa
kuendeshwa kuanzia tarehe 18 – 23 Februari, 2021 na hatimaye kuwapangia vituo
vya kazi waombaji kazi watakaofaulu usaili huo.

Wasailiwa wanaoitwa kwenye usaili   wanapaswa kuzingatia maelekezo yafuatayo:-

i. Usaili utafanyika kuanzia tarehe 18 - 23 Februari, 2021 kama ilivyoainishwa
kwenye tangazo hili;

ii. Kila msailiwa anatakiwa kufika kwenye eneo la usaili akiwa amevaa
barakoa;

iii. Kila msailiwa anapaswa kuwa na kitambulisho kwa ajili ya utambuzi;

iv. Vitambulisho vinavyokubalika ni pamoja na:- Kitambulisho cha Mkazi,
Kitambulisho cha Mpiga kura, Kitambulisho cha kazi, Kitambulisho cha Uraia
au Hati ya kusafiria;

v. Wasailiwa wanatakiwa kufika na VYETI VYAO HALISI, kuanzia cheti cha
kuzaliwa, kidato cha IV, VI, Stashahada, Stashahada ya Juu, Shahada
nakuendelea kutegemeana na sifa za Mwombaji;
vi. Wasailiwa watakaowasilisha “Testimonials”, “Provisional Results”,
“Statement of results”, hati za matokeo za kidato cha IV na VI (form IV
and form VI results slips) HAVITAKUBALIWA NA HAWATARUHUSIWA
KUENDELEA NA USAILI;

vii. Kila msailiwa atajigharamia chakula, usafiri na malazi;

viii. Kila Msailiwa azingatie tarehe na mahali alipopangiwa kufanyia usaili;

ix. Kwa waombaji waliosoma nje ya Tanzania wahakikishe Vyeti vyao vimehakikiwa na kuidhinishwa na mamlaka husika (TCU na NECTA);

x. Waombaji kazi ambao majina yao  hayakuonekana katika tangazo hili
watambue kuwa hawakukidhi vigezo, hivyo, wasisite kuomba tena pindi  nafasi za kazi zitakapotangazwa na kuzingatia mahitaji ya tangazo husika;

xi. Kwa kada ambazo wanatakiwa kusajiliwa na Bodi zao za Kitaaluma  wanapaswa kuja na vyeti vyao halisi vya usajili pamoja na leseni za kufanyia kazi; na

xii. Wasailiwa wote wahakikishe wanaingia kwenye akaunti zao na kunakili  namba ya mtihani kwa kuwa namba hizo hazitatolewa siku ya usaili.



0 comments

Post a Comment