TANGAZO LA NAFASI ZA KAZI.
Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Bukoba amepokea Kibali cha
Ajira Mbadala kwa barua ya tarehe 28 Januari, 2021 yenye Kumb. Na.
FA.170/368/01"B"/50 kutoka kwa Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya
Utumishi wa umma ha utaiwála Bora.
Kwa hiyo, anawatangazia Watanzania wote wenye Sifa na uwezo wa kujaza
nafasi 02 kama inavyoonekana hapa chini:
MSAIDIZI WA KUMBUKUMU II - (NAFASI 02) TGS B
SIFA ZA MWOMBAJI
Awe na cheti cha Astashahada (Technician Certificate - NTA LEVEL 5)
cha Utunzaji wa Kumbukumbu katika mojawapo ya fani za Afya, Masjala, Mahakama na Ardhi.
MAJUKUMU YA KAZI
Kutafuta kumbukumbu/nyaraka/mafaili yanayohitajika na wasomaji.
Kuthibiti upokeaji, uandikishaji wa kumbukumbu/nyaraka.
Kuchambua, kuorodhesha na kupanga kumbukumbu/nyaraka katika
makundi kulingana na somo husika (Classification and Boxing) kwa ajili ya
matumizi ya ofisi.
Kuweka/kupanga kumbukumbu,nyaraka katika reki (file racks/cabinets)
katika masjala/vyumba vya kuhifadhia kumbukumbu
Kuweka kumbukummbu (barua, nyaraka nk) katika mafaili.
Kushughulikia maombi ya kumbukumbu/nyaraka kutoka Serikali.
MASHARTI YA JUMLA KWA MWOMBAJI.
1. Mwombaji awe ni raia wa Tanzania na mwenye umri usiozidi miaka 45.
2. Mwombaji aambatishe nakala ya Cheti cha Kuzaliwa.
3. Maombi yote yaambatane na vyeti vya taaluma, maelezo binafsi (CV), nakala za vyeti vya kidato cha nne na kidato cha sita kwa wale waliofikakiwango Hicho na vyeti vyako kuhitimu mafunzo mbalimbali kwa kuzingatia sifa zilizoainishwa.
4.Picha moja passport size iandikwe jina kwa nyuma.
5. Hati za matokeo ya kidato cha nne na sita (Statement of Results havitakubakka).
6. Waombaji kazi ambao tayari ni waajiriwa katika nafasi za kuingilia walioko katika Utumishi wa Umma Wasiombe Kazi na wanapaswa kuzingatia maelekezo yaliyo katika Waraka Na. CAC.45/257/01/D/140 wa tarehe 30 Novemba, 2010.
7. Maombi yanaweza kyandikwa kwa lugha ya kiingereza au kiswahili.
0 comments
Post a Comment