JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA
OFISI YA RAIS SEKRETARIETI YA AJIRA
KATIKA UTUMISHI WA UMMA
Kumb. Na. EA.7/96/01/L/64
08 Machi, 2021
TANGAZO LA KUITWA KAZINI
Katibu wa Sekretarieti ya Ajira katika Utumishi wa Umma anapenda kuwataarifu
waombaji kazi themanini na tatu (83) wa nafasi mbalimbali serikalini ambao
majina yao yapo katika tangazo hili wafahamu kuwa walifaulu usaili na
kuhifadhiwa katika kanzidata (Database). Hivyo, kufuatia kufaulu kwao usaili na
kupatikana kwa nafasi wazi zinazohitajika kujazwa, wamepangiwa vituo vya kazi
katika ofisi mbalimbali katika Utumishi wa Umma.
Reccomended 💥💥💥
■■■■■■>>>>>INTERNSHIP OPPORTUNITY
Waombaji waliofaulu usaili wanatakiwa kuchukua barua za kupangiwa kituo cha
kazi katika Ofisi za Sekretarieti ya Ajira katika Utumishi wa Umma zilizo katika Chuo Kikuu cha Dodoma (UDOM) kwenye Majengo ya Dkt. Asha Rose Migiro, Masjala ya wazi ndani ya siku saba kutoka tarehe ya tangazo
hili na baada ya hapo barua ambazo hazijachukuliwa na Wahusika zitatumwa kupitia anuani zao za Posta.
■■■<<<<<< New internship opportunity>>>
Aidha, waombaji kazi waliofaulu usaili na kupangiwa kituo cha kazi wanatakiwa
kuripoti kwa Mwajiri katika muda ambao umeainishwa kwenye barua za kupangiwa kituo cha kazi wakiwa na vyeti halisi (Originals Certificates) za masomo kuanzia kidato cha nne na kuendelea ili vihakikiwe na Mwajiri kabla ya kupewa barua ya Ajira.
Kwa wale ambao majina yao hayapo katika tangazo hili watambue kuwa hawakupata nafasi/hawakufaulu usaili, hivyo wasisite kuomba kwa mara nyingine nafasi za kazi zitakapotangazwa.
■■■■■■■ BONYEZA LINK ILIYO CHINI KUPATA MAJINA. 👇👇👇👇👇
LIMETOLEWA NA;
KATIBU
SEKRETARIETI YA AJIRA KATIKA UTUMISHI WA UMMA
0 comments
Post a Comment