TANGAZO LA KUITWA KWENYE USAILI MTUWASA,TANAPA,MUHAS,UDSM 04-03-2021

 



OFISI YA RAIS SEKRETARIETI YA AJIRA KATIKA UTUMISHI WA UMMA


Kumb.Na.EA.7/96/01/L/62

04 Machi, 2021

     TANGAZO LA KUITWA KWENYE USAILI


Katibu wa Sekretarieti ya Ajira katika Utumishi wa Umma kwa niaba ya Mamlaka ya Maji Safi na Usafi wa Mazingira Mtwara (MTUWASA), Shirika la Hifadhi za Taifa (TANAPA), Chuo Kikuu Cha Afya na Sayansi Shirikishi Muhimbili (MUHAS) na Chuo Kikuu Cha Dar Es Salaam (UDSM) anapenda kuwataarifu waombaji kazi wote walioomba kazi kuwa usaili unatarajiwa kuendeshwa kuanzia tarehe 11 hadi 23 Machi, 2021 na hatimaye kuwapangia vituo vya kazi waombaji kazi watakaofaulu usaili huo.

Wasailiwa wanaoitwa kwenye usaili wanapaswa kuzingatia maelekezo yafuatayo:- 

RECCOMENDED 

i.Usaili utafanyika kuanzia tarehe 11 - 23 Machi, 2021, kama ilivyooneshwa kwenye
tangazo hili; muda na sehemu ambapo usaili utafanyika umeainishwa kwa kila
Kada;

ii . Kila Msailiwa anatakiwa kufika kwenye eneo la usaili akiwa amevaa Barakoa;

iii . Kila Msailiwa anapaswa kuwa na kitambulisho kwa ajili ya utambuzi;

iv. Vitambulisho vinavyokubalika ni pamoja na:- Kitambulisho cha Mkazi, Kitambulisho
cha Mpiga kura, Kitambulisho cha kazi, Kitambulisho cha Uraia au Hati ya
kusafiria;

v.  Wasailiwa wanatakiwa kufika na VYETI VYAO HALISI, kuanzia cheti cha
kuzaliwa, kidato cha IV, VI, Stashahada, Stashahada ya Juu, Shahada na
kuendelea kutegemeana na sifa za kada husika;

vi.  W a s a i l i w a watakaowasilisha “Testimonials”, “Provisional Results”,
“Statement of results”, hati za matokeo za kidato cha IV na VI (form V and form
VI results slips) HAVITAKUBALIWA NA HAWATARUHUSIWA KUENDELEA NA
USAILI;

vii. Kila msailiwa atajigharamia kwa chakula, usafiri na malazi;

viii. Kila Msailiwa azingatie tarehe, muda na mahali alipopangiwa kufanyia usaili;

ALSO READ 


■■■■>>>>UTUMISHI 14 NEW GOVERNMENT JOBS

ix. Kwa waombaji waliosoma nje ya Tanzania wahakikishe vyeti vyao vimehakikiwa na kuidhinishwa na Mamlaka husika (kama TCU, NACTE au NECTA);

x. Waombaji kazi ambao majina yao hayakuonekana katika tangazo hili watambue kuwahawakukidhi vigezo, hivyo, wasisite kuomba tena pindi nafasi za kazi zitakapotangazwa na kuzingatia mahitaji ya tangazo husika.

xi. Kwa kada ambazo wanatakiwa kusajiliwa na Bodi zao za Kitaaluma wanapaswa kuja na vyeti vyao Halisi vya Usajili pamoja na Leseni zakufanyia kazi.


xii. Wasailiwa wote walioitwa kwenye usaili wahakikishe wanaingia kwenye akaunti zao na kunakili namba ya mtihani kwa kuwa namba hizo hazitatolewa siku ya usaili. 


■■■■■<<<<MAJINA YA WALIOITWA KWENYE USAILI BONYEZA HAPA>>>■■■

0 comments

Post a Comment