UTUMISHI CALL FOR INTERVIEW AT TANZANIA BROADCASTING COOPERATION.

 


OFISI YA RAIS SEKRETARIETI YA AJIRA KATIKA UTUMISHI WA UMMA


Kumb.Na.EA.7/96/01/L/48
 24 Februari, 2021

TANGAZO LA KUITWA KWENYE USAILI.

Katibu wa Sekretarieti ya Ajira katika Utumishi wa Umma kwa niaba ya SHIRIKA LA UTANGAZAJI TANZANIA (TBC) anapenda kuwataarifu waombaji kazi wote walioomba
kazi kuwa usaili unatarajiwa kuendeshwa kuanzia tarehe 03 - 09 Machi, 2021 na hatimaye kuwapangia vituo vya kazi waombaji kazi watakaofaulu usaili huo.

Wasailiwa wanaoitwa kwenye usaili wanapaswa kuzingatia maelekezo yafuatayo:-


i.Usaili utafanyika kuanzia tarehe 03 - 09 Machi, 2021, kama ilivyooneshwa kwenye
tangazo hili; muda na sehemu ambapo usaili utafanyika umeainishwa kwa kila
Kada;


ii.Usaili wa Kada ya “Technician Electrical II” na “ICT Officer II” utafanyika katika kumbi
za DUCE, Co-ICT na Ofisi za TBC TAZARA Dar es Salaam na kada nyingine
zilizosalia usaili utafanyika Dodoma kwa maeneo yaliyoainishwa kwenye ratiba;

iii. Kila Msailiwa anapaswa kunukuu kwa usahihi namba yake ya usaili wa mchujo na
Vitendo, namba hizo zinapatikana kwenye akaunti ya kila Msailiwa katika mfumo wa
maombi ya kazi;


iv. Kila Msailiwa anatakiwa kufika kwenye eneo la usaili akiwa amevaa Barakoa;


v.Kila Msailiwa anapaswa kuwa na kitambulisho kwa ajili ya utambuzi;

vi. Vitambulisho vinavyokubalika ni pamoja na:- Kitambulisho cha Mkazi, Kitambulisho
cha Mpiga kura, Kitambulisho cha kazi, Kitambulisho cha Uraia au Hati ya
kusafiria;

vii. Wasailiwa wanatakiwa kufika na VYETI VYAO HALISI, kuanzia cheti cha
kuzaliwa, kidato cha IV, VI, Stashahada, Stashahada ya Juu, Shahada na
kuendelea kutegemeana na sifa za Mwombaji;

viii. Wasailiwa watakaowasilisha “Testimonials”, “Provisional Results”, “Statement
of results”, hati za matokeo za kidato cha IV na VI (form V and form VI results
slips) HAVITAKUBALIWA NA HAWATARUHUSIWA KUENDELEA NA USAILI;

ix. Kila msailiwa atajigharamia kwa chakula, usafiri na malazi;

x.Kila Msailiwa azingatie tarehe, muda na mahali alipopangiwa kufanyia usaili;

xi. Kwa waombajiwaliosoma nje ya Tanzania wahakikishe vyeti vyao
vimehakikiwa na kuidhinishwa na Mamlaka husika (kama TCU, NACTE auNECTA);


■■■■■■>>> CHECK AMAZON FIRE TV STICK HERE

■■■■■■>>>JOB VACANCIES ANNOUNCED BY TAZAMA PIPELINE LIMITED

xii. Waombaji kazi ambao majina yao hayakuonekana katika tangazo hili watambue
kuwa hawakukidhi vigezo. hivyo, wasisite kuomba tena pindi nafasi za kazi
zitakapotangazwa na kuzingatia mahitaji ya tangazo husika.

xiii. Kwa kada ambazo wanatakiwa kusajiliwa na Bodi zao za Kitaaluma wanapaswa kuja na vyeti vyao Halisi vya Usajili pamoja na Leseni
zakufanyia kazi.

xiv. Wasailiwa wote walioitwa kwenye usaili wahakikishe wanaingia kwenye akaunti zao na kunakili namba ya mtihani kwa kuwa namba hizo hazitatolewa siku ya usaili

0 comments

Post a Comment