NOTICE: NAMES CALLED FOR WORK RELEASED BY UTUMISHI TODAY 16-02-2021


 TANGAZO LA KUITWA KAZINI OFISI MBALIMBALI ZA UMMA 16-02-2021.


TANGAZO LA KUITWA KAZINI

>>>>>>■■58 NEW JOB OPENING AT TANZANIA POSTAL BANK

Sekretarieti ya Ajira katika Utumishi wa Umma inapenda kuwataarifu waombaji kazi wa nafasi mbalimbali waliofanya usaili tarehe 08 – 30 Januari, 2021 kuwa  matokeo ya waombaji kazi waliofaulu usaili huo ni kama yalivyoorodheshwa katika tangazo hili. Orodha ya majina haya pia imejumuisha baadhi ya wasailiwa  waliokuwa kwenye kanzidata (Database) kwa kada mbalimbali ambao
wamepangiwa vituo vya kazi baada ya nafasi kupatikana.

Waombaji waliofaulu usaili wanatakiwa kuchukua barua za kupangiwa kituo cha
kazi katika Ofisi za Sekretarieti ya Ajira katika Utumishi wa Umma zilizopo katika majengo ya Asha Rose Migiro yaliyomo ndani ya Chuo Kikuu cha Dodoma (UDOM), Masjala ya wazi ndani ya siku saba kutoka tarehe ya tangazo hili na baada ya hapo barua ambazo hazitachukuliwa na wahusika zitatumwa kupitia anuani zao za Posta.

Aidha, waombaji kazi waliofaulu usaili na kupangiwa kituo cha kazi wanatakiwa kuripoti kwa Mwajiri katika muda ambao umeainishwa kwenye barua za kupangiwa kituo cha kazi wakiwa na vyeti halisi (Originals Certificates) za masomo kuanzia kidato cha nne na kuendelea ili vihakikiwe na mwajiri kabla ya kupewa barua ya Ajira isipokuwa wale tu waliopangiwa Shirika la Hifadhi za Taifa (TANAPA) utaratibu wao wa kuripoti umeainishwa katika aya inayofuata.

>>>>>>>■■TRACKER JOB POSITION AT ALISTAIR GROUP APPLY JOB HERE


Waombaji kazi wote waliopangiwa kituo cha kazi Shirika la Hifadhi za Taifa (TANAPA) wanatakiwa kuripoti tarehe 25 Februari, 2021 saa 2:00 asubuhi katika ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Mpanda mkoa wa Katavi tayari kwa kuelekea katika kambi ya mafunzo ya Jeshi Usu.
Sambamba na vyeti halisi waombaji hao
waliofaulu watatakiwa kuwa na vifaa vifuatavyo vya lazima; nguo ya mazoezi
(Track Suit), Raba, Fulana, Bukta, Begi la mgongoni (Day Pack/Rucksack) na
Soksi jozi za kutosha.

>>>>>>>■■■■ TANGAZO KUITWA KWENYE USAILI MNH, SUA,TPRI,TCAA,SIDO,TALIRI, MDAs & LGAs 12-02-2021

Kwa wale ambao majina yao hayapo katika tangazo hili watambue kuwa
hawakupata nafasi/hawakufaulu usaili, hivyo wasisite kuomba kwa mara nyingine nafasi za kazi zitakapotangazwa.

■■■■■■■■■>>FOLLOW THE LINK FOR NAMES
       

0 comments

Post a Comment