Tangazo La Kazi ya Muda ya Kutenga Maeneo - Nafasi 300
TANGAZO LA KAZI YA MUDA YA KUTENGA
MAENEO - NAFASI 300
Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS) inawatangazia Watanzania wenye sifa zilizoainishwa hapo chini pamoja na afya njema kuomba kazi ya muda itakayofanyika katika mikoa yote ya Tanzania Bara ya Kutenga Maeneo kwa ajili ya maandalizi ya Sensa ya Watu na Makazi ya Mwaka 2022 (Census Geography). Muombaji awe tayari kufanya kazi katika sehemu na mazingira yoyote ndani ya Tanzania Bara.
Waombaji wanatakiwa kuwa ni watanzania wenye sifa zifuatazo;
- Umri wa miaka 18 au zaidi,
- Elimu ya Kidato cha Nne na Kuendelea mwenye uzoefu wa tafiti mbalimbali zilizofanywa na NBS,
- Elimu ya Shahada /Stashahada/ Astashahada ya Urasimu Ramani, Upimaji wa Ramani, Mipango Miji na Kozi zinazofanana na hizo watapewa kipaumbele cha kwanza.
Reccomended
■■■■>>>> 74 NEW TRANSFER VACANCIES BY MUST
Fomu ya maombi inapatikana kupitia Tovuti ya Ofisi ya Taifa ya Takwimu www.nbs.go.tz/ajira. Hivyo, muombaji apakue fomu hiyo na kuijaza kikamilifu na aitume kupitia barua pepe ifuatayo;barua@nbs.go.tz kabla ya tarehe 14 Machi, 2021 saa Tisa na Nusu Alasiri.
NB: Waombaji wote wanatakiwa kuambatisha vyeti vya taaluma na wasifu (CV). Watakaochaguliwa kwa ajili ya usaili huo watajulishwa. Aidha, NBS haitahusika na gharama zozote za kuhudhuria kwenye usaili huo.
Imetolewa Na
KAIMU MTAKWIMU MKUU WA SERIKALI
OFISI YA TAIFA YA TAKWIMU
04 Machi, 2021
0 comments
Post a Comment